Alhamisi 16 Aprili 2026 - 16:00
Shukrani za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, kutokana na mshikamano wa huzni alio uonesha Abu Alaa al-Wala’i

Hawza/ Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, kupitia ujumbe rasmi aliomtumia Abu Alaa al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Kata’ib Sayyid al-Shuhadaa, alitoa shukrani zake kwa kuonesha kwake hisia za majonzi kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, matini ya barua ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, kwa Katibu Mkuu wa Muqawama wa Kiislamu wa Kata’ib Sayyid al-Shuhadaa ni kama ifuatavyo:

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa Mheshimiwa Hajj Abu Alaa al-Wala’i (daamat tawfiiqaatukum)

السلام علیکم و رحمة ‌الله و برکاته

Kwa njia hii, tunawasilisha kwako shukrani na tathmini yetu kubwa kwa ajili ya kuonesha kwako hisia za majonzi na rambirambi kwa mnasaba wa kuuawa kishahidi Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Mwenyezi Mungu aitakase roho yake tukufu na kuifanya safi na yenye kutakasika.

Tunamuomba Mola Mtukufu akujalie mafanikio na akupe tawfiqi katika njia ya kuitumikia dini iliyo nyooka ya Uislamu.

Sayyid Mujtaba Hosseini Khamenei

Tarehe 4 Farvardin 1405 Hijria Shamsia
Sambamba na tarehe 4 Shawwal al-Mukarram 1447 Hijria Qamaria

Shukrani za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, kutokanwa na mshikamano wa huzni alio uonesha Abu Alaa al-Wala’i

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha